Photo Gallery

 • MORUWASA, WAMIRUVU KUSHIRIKIANA NA WORLD WATERNET KUHIFADHI KIDAKIO CHA NGERENGERE.

  Shirika la World Waternet Kupitia Progamu ya WaterWorx limekutana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu na kujadili mpango kazi wa pamoja wa kuhifadhi kidakio cha Ngerengere katika kikao kilichofanyika mapema leo Agosti,25,2023 katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA

  .

  Mpango kazi huo ambao unalenga kurejesha uoto katika kidakio na hifadhi ya Bwawa la Mindu unahusisha uandaaji wa mfumo wa kufanya maamuzi ili kuchagua aina ya kilimomsitu kwa kuzingatia faida za kiuchumi kwa jamii inayoishi pembezoni mwa vyanzo vya maji na faida za kimazingira.

  aasisi za TAFORI na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) pia zimeshiriki katika kikao hicho wakiwa ni wadau muhimu wa kuhifadhi mazingira katika kidakio cha Ngerengere na hifadhi ya  Bwawa la Mindu.

  Posted On : March, 23,2020

 • MORUWASA YASHIRIKISHA WADAU MAPENDEKEZO YA BEI MPYA ZA MAJI

  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) imekutana na wadau mbalimbali na kupokea maoni yao kuhusu mapendekezo ya bei Mpya za huduma za Maji kwenye kikao kilichofanyika leo Agosti 24,2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Edema, Morogoro.

  Wadau mbalimbali kutoka maeneo yanayohudumiwa na MORUWASA ya Manispaa ya Morogoro, Miji ya Kilosa na Mikumi na maeneo ya Mkambarani, Dakawa, Dumila na Mzumbe wameweza kuwasilisha maoni yao kuhusu mapendekezo ya Bei Mpya yaliyowasilishwa na MORUWASA.

  Awali akifungua kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini Mhe. Rebeca Nsemwa ameipongeza MORUWASA kwa hatua ya kushirikisha wadau na kuwataka wajumbe hao kuzingatia maslahi mapana ya wananchi katika maoni yao.

  Wadau mbalimbali walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro na viongozi wa Wilaya za Morogoro Mjini, Morogoro DC , Mvomero na Kilosa.

  Wengine ni Viongozi wa Dini Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na vyama vya upinzani, Waandishi wa Habari , Taasisi za Umma na wawakilishi wa wananchi Viwanda, Vyuo, Hoteli na wawakilishi wa mwananchi mmoja mmoja.

  Maoni yaliyotolewa na wadau yatazingatiwa katika uboreshaji wa huduma na yatawasilishwa kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuidhinisha bei mpya za huduma za maji zitakazotumika mpaka 2025/2026.

  Posted On : August,24,2023.

 • MHE. JAFO AIPA HEKO MORUWASA

  Baadhi ya watumishi wakiwa pamoja katika zoezi la ufuatiliaji bili za maji kwa watejaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo amepongeza jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) katika kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani.

  Mhe. Jafo, ametoa pongezi hizo leo Agosti 7,2023 alipotembelea Banda la MORUWASA kwenye maonesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya J.K. Nyerere mkoani Morogoro.

  Aidha, ameitaka MORUWASA kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na elimu ya kuzuia shughuli za kibinadamu zinazofanyika pembezoni mwa vyanzo vya maji ili kuepusha kujaa kwa tope katika Bwawa la mindu ambalo ni chanzo mama cha maji kwa wakazi wa Morogoro. Sambamba na hilo amesisitiza juu ya utoaji wa elimu kuhusu athari ya vitendo vya uchomaji moto wa misitu iliyopo katika Milima ya Uluguru ili kuhifadhi mazingira na vyanzo maji.

  MORUWASA inashiriki maonesho ya nanenane huku ikisogeza karibu huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka hiyo pamoja na utoaji wa elimu ya umuhimu wa utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya maji kwa wananchi wanaojitokeza katika maonesho hayo.

  Posted On : August,7,2023

 • Ziara ya katibu mkuu wizara ya maji

  Katibu mkuu akiwa na badhi ya watendaji wa MORUWASA wakati wa ziara yake alipotembele maeneo tafauti kuangalia miradi ya maji inayo endelea

  Posted On : .....