Completed Project

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MOROGORO

MIRADI ILIYOPANGWA KUTEKELEZWA KWA KIPINDI CHA MWAKA 2020-2025

 

1.Kuongeza upatikanaji wa huduma ya Majisafi katika Manispaa ya Morogoro kutoka 77% hadi kufikia 98% ifikapo mwaka 2025 kwa kutekeleza shughuli zifuatazo:

 • Upanuzi wa mtambo kutibu maji  wa Mafiga kutoka lita 27,000,000 kwa siku hadi lita 54,000,000 kwa siku na ujenzi wa bomba kuu lenye kipenyo cha 700mm kutoka Mindu hadi Mafiga .
  • Uboreshaji wa kituo cha kusukuma maji cha Tumbaku na kujenga vituo vipya vya kusukuma maji maeneo ya Mazimbu na Kigurunyembe.
  • Upanuzi wa huduma ya majisafi kwenye kata za Lukobe, Kihonda, Mkundi, Mindu, Tungi, Bigwa, Magadu, Kilakala na Kingolwira
  • Ukarabati mtandao wa majisafi maeneo ya Rock Garden, Forest, Kilakala, Boma Road na Central Business Area
  • Kuongeza uwezo wa matenki kutoka lita 10,242,500 ya sasa hadi kufikia lita 30,692, 500.00  kwa kujenga matenki 6 ya kuhifadhi maji maeneo ya Mgulu wa Ndege, Kiegea, Mafiga, Kingolwira na Lukobe
  • Kuongeza idadi ya vyanzo vya maji  na kiasi cha maji kinachozalishwa kwa kunyanyua bwawa la Mindu, kutafiti na kuvifanyia usanifu vyanzo mbadala vitakavyotosheleza mahitaji ya maji hadi kufikia mwaka 2040.
  • Ujenzi wa bomba kuu lenye kipenyo cha 700mm kutoka Turiani hadi Mkundi umbali wa 72km ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kusukuma maji.
  • Ujenzi wa bomba kuu lenye kipenyo cha 300mm kutoka Mafiga hadi birika la Mgulu wa Ndege umbali wa 16km
  • Ujenzi wa bomba kuu lenye kipenyo cha 300mm kutoka Mizani hadi birika la Mgulu wa Ndege umbali wa 8km

  2.0.Kuongeza huduma ya uondoshaji wa majitaka majumbani, maeneo ya biashara na kwenye taasisi kutoka 5% ya sasa hadi kufikia 15% ifikapo mwaka 2025 kwa kutekeleza yafuatayo:

   • Upanuzi wa mtandao wa majitaka maeneo ya Masika, Mjimpya, Rock Garden, Kichangani, Forest, Kilakala, Mazimbu na ujenzi wa mtandao mpya katika Kata zaLukobe, Kihonda na Mkundi
   • Ujenzi wa mabwawa mapya ya majitaka eneo la Kipera na kukarabati mabwawa  ya kutibu majitaka ya Mafisa na Viwandani

3.0.Kuongeza upatikanaji wa huduma ya Majisafi katika mji wa Kilosa kutoka 85.7% hadi kufikia 98% ifikapo mwaka 2025 kwa kupanua mtandao wa majisafi kwenye maeneo yasiyokuwa na huduma.
4.0. Kuongeza upatikanaji wa huduma ya Majisafi katika mji wa Mikumi kutoka 85% ya sasa hadi kufikia 98% ifikapo mwaka 2025 kwa kupanua mtandao wa majisafi kwenye maeneo yasiyokuwa na huduma kwa kufanya yafuatayo:
 • Kujenga bomba kuu lenye kipenyo cha 150-200mm umbali wa 12,918m
 • Ujenzi wa mtambo wa kutibu maji
 • ujenzi wa bomba za usambazaji zenye kipenyo kati ya 50mm hadi 125mm umbali wa 26670m
 • Ujenzi wa vituo 3 vya kusukuma maji
 • Ujenzi wa mabirika 3 yenye meta za ujazo 1500, 500, 100 maeneo ya Kidoma, Tambukareli na kukarabati mabirika mawili yenye meta za ujazo 225 na 500 yaliyoko eneo la Jeshini
 • kufunga dira 1000
 • Kukarabati vosk 73 vya kuchotea maji